Header Ads

KIBAO KATA MAANDALIZI YA HARUSI YA MAIMARTHA
Ngoma ya maandalizi ya harusi (Kibao Kata), ya Mtangazaji maarufu Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai,’ iliyofanyika juzikati licha ya kufunika vilivyo, lakini vijembe vya hapa na pale vilitawala.
Tukio hilo lilijiri Desemba 20, mwaka huu nyumbani kwa staa huyo, Namanga jijini Dar es Salaam ambapo mastaa kibao walihudhuria na kucheza ngoma ya Kibao Kata, kula na kuburudika kwa vinywaji.
Hata hivyo, katika hafla hiyo kulikuwa na vijimbe vya hapa na pale kutoka kwa baadhi ya wahudhuriaji waliokuwa wakiwananga waliovaa nguo zisizo za staha na kufanya mambo ndivyo sivyo.
Kufuatia hali hiyo, aliyekuwa mshereheshaji wa shughuli hiyo ‘MC’, Christina Manongi ‘Sintah’ aliingilia kati na kusema kama kuna mtu alikuwa na kisasi na mwenzake akamalizie nyumbani kwao na siyo pale.
“Jamani hii ni shughuli ya Maimartha na si ya mtu mwingine, hivyo kama kuna mtu ana tatizo na mtu ni bora aende kumalizia nyumbani kwake lakini siyo hapo, haihusu,” alisema Sintah.

Hata hivyo, katika hali iliyoashiria, mastaa ‘hamnazo’ wengi waliingia kati na kushindana kukata nyonga huku kila mmoja akijivunia jinsi alivyoumbwa na Muumba.
Habari na Global
Powered by Blogger.