WAREMBO WA MAISHA PLUS WAPIGA PICHA NUSU UCHI ~ Hassbaby Mapacha

WAREMBO WA MAISHA PLUS WAPIGA PICHA NUSU UCHIWarembo walioshiriki Shindano la Maisha Plus Season II, Neema Emanuel (pichani katikati) na Lucy Kessy (pichani kushoto) wameonekana kuwa mcharuko kufuatia kupiga picha chafu studio.
Kwa mujibu wa picha hizo zilizonaswa na gazeti hili wiki hii, zinawaonesha warembo hao wakiwa wamevaa blauzi juu, chini wakiwa watupu kama walivyozaliwa.

Rafiki wa karibu wa warembo hao (jina tunalo) alisema kuwa, awali wawili hao wakiwa na shosti wao (pichani kulia) ambaye si wa Maisha Plus, walikwenda kwenye studio hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kupiga picha kali za kuweka ukutani.

“Awali wakiwa na shoga yao mmoja, walikwenda studio kupiga picha kali kwa ajili ya kutundika ukutani, lakini eti ghafla wakashauriana wapige picha hizo ambazo ni za aibu,” alisema rafiki mmoja wa wawili hao.
Hata hivyo, haikujulikana sababu za warembo hao kupiga picha zenye kuchefua machoni mwa watazamaji.

Ili kujua kisa cha kupiga picha hizo, Gazeti la Risasi Jumamosi ambalo ni mahiri kwa kufuatilia hatua kwa hatua za mastaa wa Bongo, lilimvutia waya Neema ambaye alikiri.
Alisema kuwa, yeye na mashostito wake hao mara nyingi wamekuwa wakipiga picha hizo kwa ajili ya kupamba kwenye vyumba vyao.

“Hizo picha hazina maana yoyote na tumepiga kwa ajili ya faida zetu wenyewe, tunapamba kwenye vyumba vyetu na wala sioni tatizo,” alisema Neema.
Kwa upande wake, Lucy hakuwa na la kusema zaidi ya kucheka cheka tu na kukata simu.

KUTOKA : GLOBAL
Previous
Next Post »

2 comments

Click here for comments