Header Ads

BI HARUSI MAGOMENI MAPIPA AFANYA UFUSKA NA KUREKODI CD

Na Mommadou Keita
Habari kubwa iliyotawala katika Kitongoji cha Magomeni Mapipa, jijini Dar es Salaam ni kitendo cha mwanamke mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Aluwia (pichani) kufanya ufuska wa aina yake ikiwa ni siku chache baada ya kufunga ndoa, Amani linakupa A-Z.

Mwanamke huyo ambaye anadaiwa kuolewa siku chache zilizopita, alifanya vitendo hivyo vinavyotia kinyaa akiwa na mwanaume ambaye hakuweza kufahamika mara moja kisha uchafu huo kurekodiwa kwenye CD.

Gazeti hili lilifanikiwa kuinasa CD hiyo ambayo kwa sasa imezagaa katika mitaa ya Jiji la Dar huku ikigawiwa bure na baada ya kuiangalia, lilikutana na mambo ya ajabu yasiyoweza kufanywa na mtu anayejiheshimu.

Ndani ya kifaa hicho, kwa kiasi kikubwa anaonekana Aluwia akifanya ‘usodoma’ na ‘ugomora’ na mwanaume ambaye haonekani sura huku mwanamke huyo akionekana kulifurahia tendo hilo.

Wakilizungumzia sakata hilo, baadhi ya watu waliodai kumfahamu mwanamke huyo walielezea kusikitishwa na kitendo hicho na kusema kuwa, hawakuamini macho yao baada ya kumuona akifanya ufuska huo.

“Huyu (Aluwia) anaonekana kabisa alifanya ufuska huu akiwa bado ni Bi. Harusi, huoni hata hina zake bado hazijafutika, aibu iliyoje hii? Akiiona mume wake CD hii sijui ataiweka wapi sura yake,” alisema Husna mkazi wa Magomeni, Dar.

Naye Jamila, jirani wa Aluwia alisema kuwa, imekuwa ni vigumu kwake kudhani jirani yake huyo angeweza kufanya matendo hayo kwani aliamini ni mtu anayejiheshimu sana.

“Ni jirani yangu kabisa, mimi mwenyewe nilipoiona CD hii niliona aibu. Pia niliumia sana kwani nilishindwa kujua sababu ya yeye kufanya hivyo, ona sasa anaaibika yeye na ndugu zake,” alisema Jamila.

Katika kutaka kujua undani wa ishu hii, Amani lilimtafuta Aluwia kupitia simu yake ya kiganjani, alipopatikana alikuwa mgumu kutoa ufafanuzi wa kisa kizima zaidi ya kukanusha kwa kusema kuwa, anayeonekana kwenye CD hiyo siyo yeye.

“Mimi siyo Aluwia, mimi ni Asha na wala siishi Magomeni kama unavyosema bali naishi Sinza,” alidai mwanamke huyo ambaye taarifa zinadai ana mtoto mmoja.

Baada ya mwandishi wetu kumbana na kumwambia kuwa anamjua vizuri na kwamba anayeonekana kwenye CD hiyo ni yeye, Aluwia aliamua kukata simu na kuanzia hapo kila alipokuwa akipigiwa, hakupokea.

Gazeti hili linakemea vikali vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na maadili ya nchi yetu na pia linaahidi kuendelea kuifuatilia kwa undani habari hiyo na kitakachopatikana tutawaletea kwenye matoleo yetu yanayokuja.

HABARI KUTOKA ; GAZETI LA AMANI
Powered by Blogger.