Select Menu

Slider

Hassbaby Mapacha. Powered by Blogger.

Advertise

Advertise

News

Bongo Fleva

Video

Gospel

Africa

Biashara

Sikiliza wimbo mpya wa Snura akimshirikisha Nay Wamitego, wimbo unaitwa "Hawashi" Bonyeza neno Download kuupata.
DOWNLOAD

Ujio mpya wa PNC "Yule Yule" ni wimbo mpya kutoka kwake na utatoka hivi karibuni.

Sikiliza wimbo mpya wa Danny Pes Kazinda. Umetengenezwa kwenye studio ya Free Nation Studios chini ya Mr. T Touches.


Hugoline Martin Mtambachuo au unaweza kumuita DJ CHOKA aka Mr Appetite baada ya kukaa kimya kwa muda wa mwaka mmoja bila kuendelea na mix tape zake, mwaka huu amehamua kurudi tena.
Dj Choka anasema alikuwa kimya mwaka 2014 kwa kuwa alikuwa busy akimlea mtoto wake na familia yake, wimbo wa mwisho kuutoa ulikuwa unaitwa STINGA LI ambao ulikuwa umetengenezwa na Prod Pancho Latino kutoka Bhitz Music Group.
Mwaka huu 2015 Dj Choka anaanza na wimbo wake wa kwanza alioupa jina la NITALALA UZEENI huku akiwa amewashirikisha wasanii kama Country Boy, Climax Bibo, Young Lunya, Bgway na Deddy. Wimbo huu umesimamiwa na Prod mchanga anayekuja vizuri anajulikana kwa jina la GARD kutoka A.M Record.
Wimbo huu unatarajiwa kutoka siku ya Ijumaa tarehe 13 mwezi huu wa 3, na matarajio ya video yako mbioni kufanyika na kampuni ya utengenezaji video kutoka hapa hapa Tanzania.
_MG_2680
Pichani ni Dj Choka akiwa na Deddy
IMG_2636
Pichani kuanzia kushoto ni Prod Gard, Prod Maneck na Dj Choka wakiwa studio ya A.M Rec
_MG_2674
Dj Choka, Deddy, Young Lunya & Prod Gard
Kama Umeifuatilia na kuiangali Video ya Fid Q Bongo Hip-Hop Kupitia Account ya Director Nisher kwenye Youtube Basi utakuwa Shahidi kuwa Video hiyo Iliondolewa na Wamiliki wa YouTube Kitu ambacho watu wamekitafsiri Tofauti.
Taarifa za Mtaani watu wamesema eti Imefungiwa na Kampuni Flani South Africa baada ya Nisher kucopy Vitu flani kwenye Video yao.

Fid Q amefunguka ukweli kupitia Kipindi cha DUNDO cha MamboJamboRadio Arusha na kusema kuwa sababu za Video hiyo Kutolewa ni sababu yeye Fid Q amejiandikisha kabisa na anatambulika ndani ya YouTube na kuilinda Hatimiliki ya Fid Q Wao kama Youtube Wameiondoa wakidhani kuwa Nisher ni Mdananda wakati wao Wameshamuuliza Fid Q kama Video aliyoipost kwenye Account yake ya Cheusi Dawa Ni yeye na alivyowajibu ndipo Wakafungia ya Nisher bila wao Kujua kama Nisher pia anahusika kwenye HatiMiliki ya hiyo Video akiwa kama Director.
Hiyo ndiyo sababu Fid Q alomweleza @DjHaazu kuwa ndiyo issue iliyopelekea Video hiyo Kuzuiliwa kwa Masaa Kadhaa kupitia account ya Nisher
Mwanadada Chiku Ketto a.k.a Chiku K Balaa ameamua kuweka wazi hisia zake alizonazo kuhusu kile anachokiona kinamtesa Aliyekuwa Member Mwenzake wa Kundi la LaFamilia.
Akizungumza na Kipindi cha DUNDO cha MamboJambo Radio Arusha kupitia Kipengele cha DROP BOX Chiku amesema ana mpango wa kukaa Karibu zaidi na Chid Beenz Kwakuwa anajua anakoelekea sio kwema kwani wakati wakiwa Pamoja Chid alikuwa na Mafanikio na Hakuwa kama alivyokuwa Kitu ambacho kinaonekana kama Chid beenz amekosa mtu wakuwa karibu zaidi na yeye kwa Ushauri na Ukaribu wa Kimawazo Chanya.
Bila shaka mmefuatilia pia Kesi ambayo ilikuwa inamkabili Chid Beenz ambayo ilikuwa ya Kukutwa na Madawa ya Kulevya Katika Uwanja wa JK Nyerere Airport na kuachiwa huru kwa Faini ya sh. 900 000/= za Kitanzania Hivi juzi hii ni moja ya sababu zinazoonyesha Chid Baanz amefikia kubaya zaidi.
UKIWA unakumbukumbu nzuri sana utakumbuka wakati ule chid akiwa na LaFamilia Team yake hata kiafya alikuwa Kajaza na hata watu walikuwa wanamuogopa kwa kuwa alikuwa na Lile Body Flani la Kinako ila kwa sasa hata machalii wanweza kumchezea Japo Wembamba hauna maana ya kuwa Umeisha na nguvu ila kiukweli Chid Amepungua sana Kiafya.


Chiku amemshauri Chid Kuhakikisha Anakumbuka kuna Mama yake, Ndugu zake Wanamtegemea na pia Jamii nzima inamwangalia na Cha Mwisho akasema anampenda sana Chid Beenz Kuna ngoma wamefanya kwa Pamoja na Atahakikisha Kuwa Chid anaepukana na Majanga yanayomwandama.

Katika Mazungumzo hayo Chiku amepata Pia nafasi ya Kuzungumzia Ngoma zake Mbili ambazo zinatoka mwisho wa Mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi ujao Ambapo ngoma hizo mojawapo ni PIGA HATUA ambayo ilikuwa itoke mwaka jana Mwishoni lakini ikashindwa kutoka sababu alizozitaja kuwa ni Matatizo yaliyokuwa yametokea katika Management yake na Ya Pili ni ngoma ambayo itakuwa inahamasisha Vijana Kupiga Kura Ukizingatia huu ni mwaka Muafaka kwa Watanzania Kumchagua Rais Mpya, Wabunge na Madiwani katika Serikali Kuu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bonyeza HAPA kuweza ku download wimbo huu wa Isha Mashauzi "Nimpe Nani"


Tangaza Hapa

Tangaza Hapa